Home Makala Azam Fc Wajipanga Kupindua Meza

Azam Fc Wajipanga Kupindua Meza

by Sports Leo
0 comments

Baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa klabu ya Bahir Dar Kenema kikosi cha Azam Fc kimerejea nchini kujipanga kwa ajili ya kupindua meza ili kuingia hatua ya pili ya kombe la shirikisho nchini.

Katika mchezo huo wa awali ugenini Azam Fc ilikubali kichapo hicho huku ikiwa na faida ya kupata bao la ugenini dakika za mwishoni mwa mchezo likifungwa na Idriss Mbombo.

Mchezo wa marudiano unatarajiwa kufanyika jijini Dar es salaam katika uwanja wa Azam Complex Chamazi siku ya Julai 25 ambapo Azam Fc atakua mwenyeji wa mchezo huo.

banner

Afisa habari wa klabu hiyo Hashim Ibwe aliandika katika mtandao wake wa kijamii wa Instagram “Asante sana Ilunga Idris Mbombo ..!!!!! 2-1 away sio mbaya japo tumepoteza..! Chamazi Patakuwa patamu na pazito kwao tunayo nafasi ya kushinda na kusonga mbele”.

 

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited