Home Makala Azam Fc Watua Tunisia

Azam Fc Watua Tunisia

by Sports Leo
0 comments

Msafara wa kikosi cha Azam Fc umewasili nchini Tunisia kwa ajili ya kambi ya wiki tatu kujiandaa na msimu mpya wa ligi kuu ya Tanzania bara nchini pamoja na michuano ya kimataifa ambapo watashiriki michuano ya kombe la shirikisho.

Azam Fc baada ya kukamilisha usajili wake ambapo jumla imesajili mastaa watatu pamoja na kufanya mabadiliko katika benchi lake la ufundi ambapo kocha Yossouph Dabo amepewa nafasi ya kuleta wasaidizi wake.

Azam Fc msimu uliopita wamemaliza katika nafasi ya tatu ya ligi huku wakiwa hawajachukua ubingwa wa ligi kuu kwa takribani miaka 10 sasa na msimu huu ndio wana matarajio ya kuchukua ubingwa kutokana na aina ya usajili waliofanya.

banner

Kambi hiyo ya nchini Tunisia ina lengo la kutengeneza muunganiko wa kikosi tayari kwa kuipambania michuano ya ngao ya jamii ambapo wataanza kucheza na Yanga sc katika michuano ya jumla ya timu nne za Simba sc,Yanga sc na Singida Fountain Gate.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited