Singida Big Stars imekubali kipigo cha 1-0 kutoka kwa Azam Fc katika mchezo wa ligin kuu uliofanyika katika uwanja wa Azam Complex ulioko Chamazi jijini Dar es salaam bao likifungwa na Sospeter Bajana mapema dakika ya 45 za kipindi cha kwanza.
Azam Fc licha ya kuwa na matokeo mabaya katika mchezo wake dhidi ya Tanzania Prisons Fc ilifanikiwa kuonyesha mchezo mzuri na wenye mipango kiasi cha kupata matokeo katikamchezo huo wakiwabana Singida Stars katika kipindi chote cha mchezo huo na mpaka mpira unamalizika Azam Fc iliondoka na alama tatu katika mchezo huo uliowavutia wadau wengi wa soka hapa nchini.
Azam Fc kutokana na ushindi hu sasa imefikisha alama 11 katika nafasi ya sita ikicheza jumla ya michezo sita ya ligi kuu nchini huku Simba sc na Yanga sc zikiwa kileleni japo zina mchezo mmoja mkononi.