Home Makala Azam Fc Yamnasa Sopu

Azam Fc Yamnasa Sopu

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Azam Fc imekamilisha usajili wa kiungo mshambuliaji Abdul Suleiman Sopu kwa mkataba wa miaka mitatu ikishinda vita hiyo ya usajili kutoka kwa vilabu vya Yanga sc na Simba sc ambazo nazo zilipeleka ofa ya usajili kwa Coastal Union.

Sopu aliyekua na mkataba wa miaka miwili katika klabu ya Coastal Union aliousaini siku chache kabla ya fainali ya kombe shirikisho dhidi ya Yanga sc ambapo alifunga mabao matatu ‘Hatrick’ japo timu yake ilipoteza mchezo huo ambapo kuliibuka vita vikali vya usajili katika vilabu hivyo vikubwa vitatu vyote vikimnyemelea lakini ilitakiwa dau la milioni 100 kumng’oa staa huyo klabuni hapo.

Hata hivyo Azam Fc ambayo mmiliki wa klabu hiyo Yussuph Bakhresa ameamua kuingia mwenyewe katika vita ya usajili amefanikiwa kumsainisha staa huyo mkataba wa miaka mitatu huku pia kukiwa na kipengele cha kumruhusu kumuuza nje ya nchi endapo ikitokea ofa hata ya kuanza na majaribio.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited