Home Makala Azam Fc Yawatema Chilunda,Salula

Azam Fc Yawatema Chilunda,Salula

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Azam Fc imeamua kuachana na wachezaji wake wawili kipa Ahmed Salula na mshambuliaji Shabani Idd Chilunda kwa makubaliano ya pande mbili baada ya kushindwa kulishawishi benchi la ufundi la klabu hiyo yenye maskani yake Chamazi jijini Dar es salaam.

Azam Fc imefanya usajili mkubwa katika dirisha kubwa la usajili lililopita na mpaka sasa katika dirisha hilo dogo la usajili imeendelea kufanya marekebisho kadhaa ya kikosi huku tayari mbali ya kuachana na mastaa hawa tayari imeshaachana na Ibrahim Ajibu ambaye ilimsajili baada ya kuachana na Simba sc.

Katika msimamo wa ligi kuu nchini msimu huu Azam Fc ipo nafasi ya tatu ikiwa na alama 37 katika michezo 18 ya ligi kuu ikizidiwa alama kumi na vinara Yanga sc.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited