Klabu ya Azam Fc imelazimishwa suluhu na klabu ya Dodoma Jiji Fc katika mchezo wa ligi kuu nchini uliofanyika usiku huu katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.
Azam Fc ikimkosa mshambuliaje wake mahiri Prince Dube ilimuanzisha mshambuliaji mwenye mwili mkubwa Allasane Diara aliyesaidiwa na Feisal Salum,Gibri Sylla na viungo wakabaji Sospeter Bajana na Yannick Bangala walishindwa kuizidi maarifa safu ya kiungo ya Dodoma Jiji iliyoongozwa na Mtenje Albano pamoja na Gustavo Saimoni.
Kipindi cha kwanza kilimalizika kwa suluhu huku kipindi cha pili licha ya jitihada za walime Melis Medo na Yousouph Dabo kufanya mabadiliko bado hayakuzaa matunda na kusababisha mpaka dakika tisini kumalizika kwa matokeo hayo.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Kutokana na hilo sasa Azam Fc imefikisha alama 10 katika michezo minne ya ligi kuu ikishinda mitatu na suluhu moja huku Dodoma Jiji ikifikisha alama 5 katika michezo minne ya ligi kuu ya Nbc nchini.