Klabu ya Azam imetumia ndege binafsi kumleta jijini Dar es salaam beki wake wa kulia, Nicolas Wadada aliyekuwa amekwama nchini kwao Uganda kutokana na uwepo wa zuio la kutotoka nje na kufungwa kwa mipaka kwa ajili ya kukabiliana na virusi vya Corona.
Azm fc imelazimika kufanya hivyo kutokana na umuhimu wa beki huyo kuelekea mchezo wa ligi kuu Tanzania bara dhidi ya Mbao fc utakaofanyika jijini Dar es salaam.
Wadada amejihakikishia namba ya kudumu katika kikosi hicho kinachonolewa na kocha Aristica Cioaba ambapo hutumika kama mlinzi wa upande wa kulia.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.