Home Makala Azam,Bajana Mambo Safi

Azam,Bajana Mambo Safi

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Azam Fc ipo mbioni kumuongezea mkataba mpya wa miaka miwili kiungo wake Sospeter Bajana baada ya huu uliopo kuelekea tamati ifikapo mwishoni mwa msimu huu wa ligi kuu nchini.

Pamoja na Taarifa za kiungo huyo kuhitajika na klabu ya Simba sc klabu hiyo imefanikiwa kukubaliana kimaslahi na kiungo huyo kuhusu mkataba mpya wa miaka miwili huku pia kukiwa na juhudi kwa watu wanaosemekana kuwa wa Simba sc kumshawishi staa huyo ajiunge nao.

Bajana ambaye pia ni nahodha wa Azam Fc amekua na kiwango kizuri eneo la katikati mwa uwanja akishirikiana vizuri na James Akaminko kiasi cha kuifanya timu hiyo kumasimama katika nafasi ya tatu ya msimamo wa ligi kuu nchini ikiwa na uhakika wa kushiriki michuano ya kimataifa msimu ujao huku pia ikifanikiwa kuingia hatua ya fainali ya michuano ya kombe la shirikisho la Azam hapa nchini.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited