Site icon Sports Leo

Aziz Ki Kutimka Yanga Sc

Uongozi wa Klabu ya Yanga Sc umethibitisha kwamba kiungo mshambuliaji wao, Stephine Aziz Ki atajiunga na klabu ya Wydad Casablanca baada ya klabu hiyo kumalizana na Yanga sc kwa dau ambalo halijawekwa wazi.
Wydad Athletic Club ambao wanashiriki michuano ya klabu bingwa duniani kwa upande wa vilabu kuanzia mwezi juni tayari wameanza maboresho ya kikosi chao ambapo Aziz Ki ni mmoja ya mastaa waliopo katika mipango hiyo.

Tayari klabu hiyo imeshafikia makubaliano binafsi na staa huyo ambapo sasa makubaliano na klabu hiyo kuhusu dau la usajili yakiwa yamefikia pazuri sana.

Wydad wanamhitaji staa huyo kujiunga na kambi ya maandalizi ya michuano hiyo inayoanza leo Juni 19 ambapo Aziz tayari amesharuhusiwa na Yanga sc na mchezo wa jana dhidi ya Jkt Tanzania ndio mchezo wa mwisho wa staa huyo klabuni hapo.

Yanga sc walimpa unahodha kama ishara ya kumuaga staa huyo kikosini humo kutokana na nidhamu kubwa aliyoionyesha kwa miaka mitatu aliyokaa klabuni hapo.

Tayari Yanga wameshatengeneza video za kumuaga nyota huyo na wiki ya kuanzia kesho wataziachia ambapo pia Aziz Ki atasafiri kwenda Morocco.

Exit mobile version