Timu ya wanawake ya klabu ya Simba sc(Simba queens) imeifunga timu ya wanawake ya Yanga Princess mabao 5-1 katika mchezo wa ligi kuu uliofanyika jijini Dar es salaam.
Simba Queens ilipata mabao yake kupitia kwa mshambuliaji hatari Mwanahamisi Omary dakika ya 32 na 75 na
Oppah Clement dakika ya 65 na 82 ambao walifunga huku bao jingine lilifungwa na Joelle Bukuru dakika ya 69.
Joel Nasri dakika ya 35 alipachika bao pekee la Yanga Princess ambayo imepanda ligi msimu uliopita ikiwa haijabahatika kupata ushindi mbele ya Simba.
Ushindi wa Simba queens ni kama salamu kwa kikosi cha Yanga sc wanaume ambao watakutana na Simba sc katika mchezo wa kombe la shirikisho siku ya Jumapili.