Shirikisho la Soka Afrika limetangaza bao lililofungwa na Pape Sakho wa Simba kwenye mechi dhidi ya Asec Mimosas kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es salaam kuwa bao bora la wiki katika mechi za raundi ya kwanza hatua ya makundi Kombe la Shirikisho Afrika.
Sakho alifunga bao hilo dakika ya 12 ya mchezo huo wa kwanza kwa Simba sc hatua ya makundi ya kombe la shirikisho akipokea pasi ya upendo kutoka kwa Shomari Kapombe na kufunga kwa Tiktak akiruka kupiga mpira kuelekea nyuma na kufunga katika mchezo ulioisha kwa Simba sc kushinda 3-1.
Sakho aliyesajiliwa kutoka klabu ya Teungueth Fc inayoshiriki ligi kuu nchini Senegal amekua na kiwango cha kupanda na kushuka tangu ajiunge na ligi kuu nchini huku majeraha yakiwa yanamuandama mara kwa mara na kumfanya awe na kiwango imara.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.