Xavi Hernandez anaripotiwa kupewa dili la kuinoa timu ya Barcelona kwa kipindi cha miaka miwili akichukua nafasi ya Ernesto Valverde.
Mtendaji mkuu wa Barcelona Oscar Grau na kiongozi Eric Abidal wameonekana kufanya mazungumzo na nyota huyo wa zamani.
Ni mara baada ya kupokea kichapo cha mabao 3-2kutoka kwa Atletico Madrid kwenye nusu fainali ya kombe la Super Cup, Saudi Arabia.
Kutua kwa kocha Xavi ndani ya Barcelona kutampa wakati mgumu wa kuitengeneza timu upya na kuweza kunyakuwa taji la nane la La Liga.
Wengine wanaotajwa kutua Barcelona ni Pep Guardiola kocha wa Manchester City na Thlery Henry.