155
Beki mtanzania anayekipiga ndani ya klabu ya Nkana nchini Zambia, Hassan Kessy yupo kwenye mjadala wa Kamati ya usajili wa Yanga na jina lake limekabidhiwa kwa Kocha Mkuu wa timu hiyo Luc Eymael.
Kessy ni mchezaji huru hivi sasa kwa mujibu wa kanuni za Fifa kutokana na mkataba wake kumalizika Agosti mwaka huu hivyo anaruhusiwa kufanya mazungumzo na klabu nyingine itakayomhitaji.
Jina la beki huyo wa pembeni limependekezwa na uongozi wa Yanga ili kuiboresha safu hiyo ya beki wa pembeni inayochezwa hivi sasa na Juma Abdul na Paul Godfrey ‘Boxer’ ambaye hana nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza.
Luc Eymael anamtaka beki mwenye uwezo na uzoefu wa kucheza michuano ya kitaifa na kimataifa hivyo uwezekano mkubwa wa Kessy kusajiliwa na Yanga upo kwani mchezaji huyo pia yupo tayari kujiunga na timu yoyote itakayomfata kiofisi .
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.