Mlinzi wa zamani wa Ivory Coast ‘Sol Bamba’ amepatikana na Non-Hodgkin lymphoma ambayo saratani inayoathiri mfumo wa Lymph – Lymphatic system (Mfumo wa kinga ni mkusanyiko wa viungo, seli na tishu maalumu ambazo zinafanya kazi pamoja ili kulinda mwili dhidi ya bakteria na virusi vimelea)
Ugonjwa huo humfanya achoke kila wakati, atapunguza uzito haraka na kuwa na maumivu mengi ya mgongo na uvimbe,Sol mwenye umri wa miaka 35 aliwahi kushiriki kwa Tembo hao wa Ivory kwenye Olimpiki ya Beijing 2008 na AFCON 2012 akiwa na mastaa mbalimbali wa enzi hizo Didier Drogba na wengineo.