Licha ya dili kuvurugika dakika za mwishoni msimu uliopita klabu ya Yanga sc imerudi katika mbio za kumsajili beki Erick Rutanga ambaye ilighairi kumsajili dakika za mwishoni Msimu uliopita.
Inadaiwa kuwa klabu hiyo haijaridhishwa na kiwango cha Adeyum Salehe hivyo inafikiria kuachana nae katika dirisha dogo na imeanza kumtafuta beki huyo anayekipiga Polisi Sc ya nchini Rwanda.
“Nikiwa Rayon Sports nilitakiwa nijunge na Yanga ambao tayari tulikuwa tumeshakubaliana kwa mambo mengi lakini mwisho wa siku mambo hayakunyooka.
“Katika dirisha hili dogo la usajili naona Yanga wamerudi tena, hivyo siwezi kuzungumza lolote juu ya hili jambo, tutaona litakavyokuwa,” amesema beki huyo.