Site icon Sports Leo

Ben McCarthy Hali Tete Kenya

Aliyekuwa mchezaji wa Manchester United Benni McCarthy anaendelea kusubiri ushindi wake wa kwanza kama kocha wa Timu ya Taifa ya Kenya Harambee Stars kufuatia sare tasa dhidi ya Chad kwenye mchezo wa kimataifa wa kirafiki katika dimba la Marrakech, Morocco.

Huu unakua mchezo wa tatu kwa kocha huyo raia wa Afrika ya kusini tangu alipopewa jukumu la kuifundisha nchi hiyo machi mwaka huu ambapo mchezo wake wa kwanza dhidi ya Gambia alitoa sare ya 3-3 kisha akakubali kipigo cha 2-1 dhidi ya Gabon na sasa ametoa suluhu dhidi ya Chad.

Matokeo hayo yanazidi kuzua hofu kwa mashabiki wa Harambee Stars kutokana na kuwa na imani kubwa na kocha huyo.

Akiwakosa mastaa wake wengi mccarthy alianza na kipa Brian Bwire anayeichezea Polokwane City ya Afrika Kusini huku mabeki wakiwa ni Daniel Sakari,Aboud Omar,Alphonce Omija na Brian Mandela huku kiungo wakiwa ni Alpha Onyango,Brian Musa na Boniface Muchiri na washambuliaji wakiwa ni William Lenkupae,Adam Wilson na Moses Shumah.

Harambee Stars waliumiliki mchezo huo kwa asilimia kubwa huku wakikosa nafasi kadhaa za mabao kupitia kwa Lenkupae na Shumah.

Mpaka dakika 90 zinamalizika matokeo yalibaki suluhu ambapo timu hizo zinarudiana tena kesho ikiwa ni maandalizi ya kuelekea michuano ya Chan mwezi Augusti.

Exit mobile version