Bondia Maxim Dadashev 28 raia wa Urusi amefariki baada ya kupata majeraha alipokua ulingoni katika pambano la raundi 12 dhidi ya Subriel Matias siku ya ijumaa nchini humo.
Bondia huyo alipambana mpaka raundi ya 11 na licha ya kupigwa makonde mazito bado aligoma kutoka ulingoni hali iliyomfanya mmoja ya walimu wake kurusha taulo ulingoni ishara inayoashiria kumaliza pambano katika jitihada za kumsaidia Dadashev.

Bondia Dadashev akipokea matibabu ulingoni baada ya moja ya walimu wake kurusha taulo ili kumuokoa asiendelee na pambano.
“Kama unavyofahamu ngumu moja inaweza kubadili maisha yote ya kijana na nilikuwa siwezi kuruhusu hilo litokee”Alisema James Mcgirt mmoja ya walimu wa bondia huyo.
Inadaiwa baada ya pambano kusimamishwa bondia huyo alitapika wakati akielekea vyumbani hali iliyolazimu kubebwa na gari la wagonjwa(Ambulance) mpaka hospitali ya Um Prince George Hospital Center alipowekwa katika koma na taratibu za kumfanyia upasuaji kuanza baada ya kugundulika damu imevilia katika ubongo.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Dadashev ni mzaliwa wa St Petesburg nchini Urusi na alikua bondia wa kulipwa mwenye rekodi ya kucheza mapambano mapambano 14 na kupoteza moja(13 bila kupoteza).