Bunge limeipongeza Klabu ya Simba kwa kufuzu hatua ya Robo fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF), ikiwa ni siku chache baada ya kuibanjua AS Vita ya DR Congo kwa mabao 4-1.
Akitoa pongezi hizo bungeni jijini Dodoma, Naibu Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson, alisema kuna wabunge yawezekana hawajaelewa uzito wa ushindi huo wa Simba.
“Ni jambo ambalo sisi kama taifa tunapaswa kuungana kuwatia moyo wachezaji wetu na klabu yetu iendelee kufanya vizuri kwa sababu inapata fursa ya kuitangaza nchi yetu vizuri,” alisema.
Dk.Tulia alisema “Naamini mashabiki wa Yanga wataungana nami katika pongezi hizi kwa klabu ya Simba.”