Home Makala Carlinhos Aanza Mazoezi Rasmi Yanga

Carlinhos Aanza Mazoezi Rasmi Yanga

by Sports Leo
0 comments

Carlos Stenio Fernandez Guimaraes ‘Carlinhos’ambaye ni kiungo kipya ndani ya Yanga Sc ameanza kujifua rasmi ndani ya kikosi chake jana mara baada ya kumalizana na uongozi wa yanga katika hatua za usajili.

Yanga Sc ilianza mazoezi Agosti 10, Uwanja wa Chuo cha Sheria ikiwa ni kwa ajili ya maandalizi ya ligi kuu bara inatarajiwa kuanza Septemba 6 ambapo mchezo wa kwanza kwa Yanga itakuwa dhidi ya Tanzania Prisons, Uwanja wa Mkapa.

Carlinhos ameonekana akiwa ni mwenye furaha mazoezini baada ya kukaribishwa na wachezaji wenzake ambao tayari walishaanza mazoezi ikiwa ni pamoja na Tuisila Kisinda, Tonombe Mukoko.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited