Ilibaki kidogo tu Manchester United iadhirike ugenini baada ya kulazimika kusawazisha mbao mawili ya Southampton yaliyofungwa mapema kipindi cha kwanza na Jan Bednarek dakika ya 23 na James Ward-Prowse dakika ya 33 kwa faulo.
Bruno Fernandes alifunga bao la kwanza dakika ya 60 akipokea pasi ya Cavani kisha dakika ya 74 na 90+2 Edson Cavani alisawazisha na kuongeza bao la ushindi kwa mipira ya vichwa na kuwafnya United kuchukua alama tatu ugenini.
Ushindi huo umeifanya Man United kupaa mpaka nafasi ya nane kwenye msimamo wakiwa na alama 16 huku Tottenham akiwa kileleni na alama 21 lakini United wana mchezo mmoja mkononi.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.