Uongozi wa Simba Sc umemtangaza mtendaji mkuu mpya wa klabu yao(CEO), Barbara Gonzalez ambaye atakuwa mrithi katika kiti cha Senzo Mbatha ambaye alijiuzulu na kuibukia Yanga Sc.
Mkurugenzi wa bodi ya wakurugenzi Simba Sc,Mohamed Dewji amesema kuwa makubaliano hayo yamefikiwa jana na viongozi kwenye kikao cha bodi ya wakurugenzi.
Gonzalez anakuwa CEO wa kwanza wa kike ndani ya Bongo kuitumikia klabu ya Simba Sc kwa msimu wa 2020/2021.