Taarifa zinaeleza kuwa Chelsea ipo tayari kumtoa kipa wao namba moja, Kepa Arrizabalaga kwa mkopo baada ya kumpata mbadala wake ambaye ni Edouard Mendy kutoka klabu ya Rennes.
Inaelezwa kuwa sababu ya Lampard kutaka kumtoa kwa mkopo kipa huyo ni ili aweze kuwa imara huko atakokwenda kwa kuwa hatakuwa na nafasi ndani ya kikosi cha Chelsea kwa wakati ujao.
Kocha huyo wa Chelsea amempa dili la miaka mitano Mendy kwa kiasi cha Euro milioni 22 na dili hilo lilikamilika jana Septemba 24.