Home Makala Chelsea, Mabao Kama Mvua

Chelsea, Mabao Kama Mvua

by Sports Leo
0 comments

Everton ilikutwa jana na mvua ya mabao mengi kutoka Chelsea na kujikuta wakilowana na kutetemeka kwa baridi ya mabao 4-0 katika uwanja wa Stamphord Bridge,mchezo uliosimamiwa na refa kutoka England Kelvin Friend.

Bao la kwanza la pekee lilifungwa dakika ya 14 kupitia Mason Maunt likifuatiwa na bao la pili kutoka kwa Pedro dakika ya 21 katika kipindi cha kwanza cha mchezo.

Kipindi cha pili dakika ya 51 Willian aliongeza bao la tatu kwa Chelsea na furaha ya mashabiki ilizidi pale Olivier Giround  alipofunga bao la nne.

banner

Mchezo huu unaipa Chelsea pointi 48 ikiwa nafasi ya nne katika mechi 29 alizocheza sambamba na Everton iliyo nafasi ya 12 ikiwa na pointi 37 kibindoni.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited