Home Soka Chukwu,Fikirini Warejea Singida Bss

Chukwu,Fikirini Warejea Singida Bss

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Singida Black Stars imewarejesha wachezaji Morice Chukwu na Fikirini Bakari waliokua kwa mkopo katika klabu za Tabora United na Fountain Gate Fc.

Mastaa hao mwanzoni mwa msimu huu walitolewa kwa mkopo katika klabu hizo kwa ajili ya kuboresha viwango vyao huku kuwapa nafasi zaidi ya kucheza lakini Chukwu ambaye alikua panga pangua katika kikosi cha Tabora United aliwavutia mabosi wa klabu hiyo kumrejesha ili kutoa changamoto ya kupambania nafasi kwa viungo waliopo klabuni hapo.

Kwa upande wa Fikirini Bakari amerejea klabuni hapo baada ya kuingia matatizoni na mabosi wa Fountain Gate Fc ambapo ilifikia hatua akasimamishwa lakini baada ya kuondoka kwa golikipa Mohammed Camara ambaye ametolewa kwa mkopo wa miezi sita katika klabu ya Pamba Jiji kumemhakikishia nafasi ya kurejea klabuni hapo.

banner

Singida Black Stars kesho itavaana na Simba sc katika uwanja wa Liti ambapo mastaa hao wana uhakika wa kuwa katika kikosi cha wachezaji 21 watakaoanza katika kikosi cha mchezo huo kutokana na nafasi zao katika klabu hiyo.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited