Klabu ya Real Madrid ilikua katika nafasi nzuri ya kukamilisha usajili wa Mshambuliaji Kylian Mbappe kutoka Psg kwa mujibu wa kuingo wa zamani wa klabu ya Psg Jerome Rothen.
Inadaiwa kocha Zinedine Zidane anamhitaji mshambuliaji huyo kwa udi na uvumba ili kuboresha safu ya ushambuliaji ambayo imeyumba tangu kuondoka kwa Cristiano Ronaldo lakini janga la Virusi vya Corona ndio linalichelwesha dili hilo.
Mbappe ana mkataba na Psg mpaka mwaka 2022 lakini haonyeshi dalili za kuongeza mkataba licha ya juhudi za klabu hiyo kumshawishi aongeze.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.