Kiungo wa zamani wa Klabu ya Manchester United,Marouane Fellaini ambae kwa sasa anakipiga ndani ya Klabu ya Shandong Luneng ya China amegundulika kuwa na virusi vya Corona.
Nyota huyo mwenye miaka 32 anakuwa mchezaji wa kwanza ambaye anashiriki ligi kuu China kugundulika kuwa mwenye virusi vya Corona siku ya Ijumaa katika hospitali iliyopo mjini Jinan na mpaka anagundulika hakuonyesha dalili zozote kwamba hayupo salama.
Fellain amesema anawashukuru mashabiki kwa kuwa naye bega Kwa bega naye pia anaamini atarejea kwenye shughuli zake kama kawaida kutokana na huduma anazopata kwa madaktari wa Jinan.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.