Kipa namba moja wa Azam FC,David Kissu ameweka rekodi ya kuwa kipa pekee ligi kuu bara baada ya kucheza dakika 360 sawa na mechi nne bila kuruhusu bao lolote.
Kissu alijiunga na Azam FC, akitokea Gor Mahia ya Kenya alipokipiga kwa mafanikio makubwa akifanikiwa kutwaa ubingwa wa ligi kuu nchini Kenya mara mbili.
Kisu amekusanya ‘clean sheet’ hizo kwenye mechi dhidi ya Polisi Tanzania, Coastal Union, Mbeya City na Tanzania Prisons ambapo amecheza kwa dakika 90 kwenye mechi zote.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Azam Fc inashika nafasi ya kwanza ligi kuu bara ikikusanya jumla ya pointi 12, kwenye mechi nne walizoshuka dimbani huku wakifunga jumla ya mabao matano na wakiwa hawajaruhusu bao lolote hadi sasa.