Site icon Sports Leo

Diarra Atwaa Tuzo

Golikipa wa Klabu ya Yanga sc Djigui Diarra ameshinda tuzo ya mchezaji bora Afrika msimu 2023 | 24, tuzo hizi hutolewa nchini Mali kwa wachezaji wao waliofanya vizuri kwa msimu husika (Mali Football Awards).

Kipa huyo namba moja nchini Tanzania ametwaa tuzo hiyo akiwashinda wachezaji wenzake Aliou Dieng wa Al-Ahly ya nchini Misri, Sadio Kanoute wa Simba Sc, Fily Traore  wa TP Mazembe na Abdoulaye Kanou wa USM Alger ya nchini Algeria.

Diarra amewapiku baada ya kufanya vizuri zaidi nchini Tanzania akiwa na klabu yake ya Yanga sc ambapo ameisaidia klabu hiyo kutwaa taji lake la 30 la ligi kuu ya soka ya Nbc huku likiwa taji la tatu mfululizo huku pia akiwa ameifikisha timu fainali ya kombe la Shirikisho la Crdb.

Pia Diarra msimu uliopita alifanikiwa kutwaa tuzo ya kipa bora na tayari msimu huu mpaka sasa amepata clean sheet 15 nyuma ya Loy Matampi wa Coastal Union mwenye 16 lakini Diarra amepata hizo akiwa na michezo michache zaidi ya Matampi.

Mpaka sasa haijaeleweka mstakabari wa kipa huyo klabuni hapo kama ataendelea ama kusalia ama atatafuta malisho mapya kutokana na kuwa na kiwango bora zaidi huku akiwa na uhakika wa nafasi katika kikosi cha timu ya Taifa ya Mali.

Exit mobile version