Taarifa za uhakika zinaeleza kuwa klabu ya Simba sc ina hatihati ya kukamilisha dili la staa wa zamani wa Vipers Fc ya nchini Uganda Cesar Manzoki kukipiga kwenye klabu yao kutokana na timu yake ya sasa ya Fc Dilian ya nchini China kuvutiwa na huduma yake na kuamua kuweka Ofa kubwa mezani.
Mabosi wa Dilian baada ya kumuona katika mechi kadhaa alizocheza wameamua tayari kuanza mazungumzo na mshambuliaji huyo kuhusu dili jipya ambapo wamekubaliana atasaini mkataba mwingine wenye thamani kubwa na mshahara ambao ni mrefu zaidi ya ule wa awali.
Inaelezwa mshahara wa Manzoki kwenye mkataba wake mpya huko China atavuta takribani Sh60 milioni kwa mwezi kama mshahara na ile hela ya kusaini mkataba ni zaidi ya Simba iliyokuwa tayari kumpatia.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Kutokana na Manzoki kuwa na uhakika wa kusaini mkataba mpya huko China, chanzo kinasema atakuja nchini mwezi huu kufanya kikao na Mabosi wa Simba ili kuwaeleza masilahi makubwa anayopata huko na kuona kama watapandisha ofa yao.