Dili la aliyekua beki wa klabu ya Yanga sc Djuma Shabani kujiunga na Azam Fc limekwama rasmi baada ya dili la Mlinda lango wa Azam Fc Ali hamada kujiunga na moja ya klab inayoshiriki ligi kuu ya Sudan kukwama Katika dakika za mwisho hivyo kusababisha Usajili wa Djuma Shaban kushindwa kukamilika ndani ya Azam kwakuwa orodha ya wachezaji wakigeni itakuwa imezidi.
Azam Fc ilitegemea kumtoa Ali hamada kujiunga na moja ya klab inayoshiriki ligi kuu ya Sudan ili ipate nafasi ya kumsajili Djuma shaban ambaye kwasasa ni Mchezaji huru katika dakika za lala salama kabla ya kushindikana kutokana na Usajili wa Ali ahamada kushindwa pia kukamilika katika dakika za lala salama kabla ya dirisha la usajili kufungwa usiku wa kuamkia leo.
Kutokana na kukwama kwa usajili huo sasa Djuma shaban itabidi aendelee kusubiri hadi dirisha dogo la usajili la mwezi januari ili kukamilisha usajili huo ndani ya matajiri hao wa Chamazi
Akizungumza na waandishi wetu mkuu wa Idara ya habari ya klabu hiyo Zakaria Thabit alisema kuwa klabu hiyo ilishafunga usajili siku nyingi hivyo dili hilo halikuwepo “Azam usajili tulifunga tangu 30 July 2023, hizo taarifa za Djuma Shabani sio za kweli”.
Awali ilisemekana kuwa Djuma pamoja na Yannick Bangala walikua na mpango wa kuondoka Yanga sc kujiunga na Azam Fc ambapo Yannick alifanikiwa kufanikisha dili hilo mapema ambapo alijiunga kwa dau la shilingi milioni 100 za kitanzania huku Djuma aliendelea kusubiri hatma yake na mabosi wa Yanga sc ambapo walimalizana wiki moja iliyopita hivyo kusababisha dili hilo kuchelewa.