Home Makala Djuma,Yanga sc Mambo Safi

Djuma,Yanga sc Mambo Safi

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Yanga sc imemalizana kwa amani na beki raia wa Kongo Drc Djuma Shabani baada ya kumpatia barua ya kumuacha huru baada ya mvutano wa muda mrefu baina yao.

Djuma Shabani aliyetua nchini kwa mbwembwe nyingi baada ya kufanya vizuri na As Vita Club ya nchini kwa Kongo alikua amesaliwa na mkataba wa mwaka mmoja klabuni hapo lakini kutokana na madai ya uongozi wa klabu hiyo kuwa na tatizo la utovu wa nidhamu klabu hiyo iliamua kuachana nae.

Tatizo zaidi lilianza pale beki huyo alipowasilisha barua ya kuvunja mkataba ambapo kwa ndani lengo likiwa ni kuboreshewa maslahi yake lakini klabu hiyo iliamua kuachana nae huku ikimpa masharti ii kuvunja mkataba huo.

banner

Mvutano baina yao ilikua na namna ya kumalizana hasa katika baadhi ya vipengele ikiwemo kutojiunga na timu yeyote hapa nchini ndio vilikua vinasumbua zaidi.

Sasa tayari suala hilo limefika tamati ambapo mchezaji huyo ameshakabidhiwa barua ya kuachwa (Release Letter) na sasa anaweza kujiunga na klabu yeyote iwe nchini ama nje ya nchi.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited