Hatimaye klabu ya Azam Fc imeridhia ombi la kuvunja mkataba kwa mshambuliaje wake Prince Dube baada ya kukamilisha vipengele vya kimkataba ikiwemo kulipa kiasi kilichotakiwa ili awe huru kuondoka klabuni humo.
Haikua rahisi kwa klabu hiyo kuridhia ombi la staa huyo kuondoka klabuni hapo lakini baada ya purukushani za hapa na pale lakini imebidi kukubaliana na ombi hilo hasa baada ya mchezaji huyo kugoma kutolewa kwa mkopo ama kuuzwa akitaka awe huru.
Taarifa rasmi kutoka klabuni hapo kwenda kwa mashabiki mbalimbali inasema kuwa klabu hiyo imekubali kuvunja mkataba huo baada ya mchezaji huyo kukubali kukamilisha matakwa ya kimkataba ambapo ilimlazimu mchezaji huyo kulipa kiasi cha dola laki tatu ili kuwa huru japo kuna taarifa zinasema kuwa busara ilitumika ambapo mchezaji huyo amelipa dola laki mbili pekee.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Kutokana na mchezaji huyo kumalizana na Azam Fc sasa ni wazi anakwenda kujiunga na Yanga sc ambao tangu mwanzo walikua wanatajwa kuwa ndio sehemu ambayo staa huyo ana mpango wa kwenda kucheza ili kukidhi kiu yake ya kutwaa makombe.