Home Makala Fagio la Chuma Lapita Azam Fc

Fagio la Chuma Lapita Azam Fc

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Azam Fc imeendelea na mpango wake wa kusafisha kikosi hicho ili kuleta mastaa wapya klabuni tayari kupigania ubingwa wa ligi kuu na michuano ya kimataifa kuanzia msimu ujao ambapo licha ya kufanya usajili wa kocha mpya pamoja na kiungo Feisal Salum imeendelea kusafisha pia katika maeneo kadhaa.

Leo hii klabu hiyo imethibitisha kumalizana na kocha wa makipa Dani Cadena ambaye alikua anakaimu kama kocha mkuu baada ya Kally Ongala kukosa sifa za kuwa kocha mkuu.

Cadena aliyejiunga na klabu hiyo msimu uliopita ameondolewa kupisha safu mpya ya benchi la ufundi chini ya kocha Youssouph Dabo ambaye aliwasili klabuni hapo mapema ili kusoma mazingira na kufanya usajili wa mastaa wapya.

banner

Mbali na kocha huyo pia mastaa watatu Kenneth Muguna,Rogers Kola na Bruce Kangwa ambapo inatarajiwa kuwa mastaa wa maana watatua klabuni hapo kuchukua nafasi hizo.

Azam Fc msimu huu imemaliza katika nafasi ya tatu ya ligi kuu ya Nbc na inapambana kuanza ujenzi wa kikosi mapema ili kujiandaa na michuano ya ngao ya jamii itakayoshirikisha timu nne kuanzia msimu ujao ambapo Simba sc,Yanga sc pamoja na Singida Fountain Gate zitashiriki huku pia ikiwa na tiketi ya kushiriki kombe la shirikisho barani Afrika.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited