Winga wa Yanga, Farid Mussa amefichua kwa kusema mashindano ya Chan huko Cameroon kwake ni fursa ambayo anaitumia kuonyesha kipaji chake ili arejee kucheza soka la kulipwa barani Ulaya.
Awali Farid alikuwa akiichezea CD Tenerrife ya Hispania lakini kutokana na mambo ambayo yalikuwa nje ya uwezo wake ilibidi arejee nyumbani Tanzania ili kuweka mambi sawa kisha kuanza moja kupigania ndoto zake.
Akiwa Cameroon amesema:
“Najisikia furaha kuwa sehemu ya alama tatu ambazo tumezipata. Kwangu hii ni fursa kuonyesha kipaji changu natambua mawakala mbalimbali wakubwa wanafuatilia mashindano haya.”
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Farid amesema shauku yake ni kuona wanavuka hatua ya makundi na kuonyesha Afrika kuwa Tanzania ni taifa la mpira, “Naamini tuna nafasi ya kusonga mbele.
Cc:Kibezedon