Klabu ya Yanga sc leo imempokea mshambuliaji wao mpya Fiston AbdulRazak ambaye amewasili kujiunga rasmi na timu hiyo baada ya kusajiliwa katika usajili wa dirisha dogo.
Mshambuliaji huyo raia wa Burundi ametua leo mchana katika uwanja wa ndege wa J.K.Nyerere na kupokelewa na mashabiki wengi kama ilivyo mila na destruri ya klabu hiyo pindi mchezaji mpya anapotua kwa mara ya kwanza.
Viongozi kadhaa wa Yanga sc akiwemo makamu mwenyekiti wa kamati ya usajili injinia Hersi Said pamoja Afisa mhamasishaji Antonio Nugaz walikuwepo kumpokea mchezaji huyo.