Mchezaji kinda wa timu ya taifa ya England Phil Foden huenda akauokosa mchezo wa fainali wa michuano ya Euro 2020 kutokana na maumivu ya mguu. Foden alianza katika michezo miwili ya awali ya hatua ya makundi kabla ya nafasi yake kuchukuliwa na Bukayo Saka katika michezo iliyofuata.
Kocha wa England Southgate amesema”Phil amepata majeraha kidogo hivyo tuna wasiwasi kama atahusika na mchezo wa fainali”.
England itamenyana na Itali katika fainali ya michuano ya Euro 2020 Julai 11 itakayofanyika katika dimba la Wembley London nchini England.