Klabu ya Azam Fc imemsajili kipa Issa Fofana kutoka klabu ya Al Hilal Fc ya nchini Sudan kwa mkataba wa miaka miwili kuja kumpa changamoto kipa Aishi Manula kuelekea msimu ujao wa ligi kuu na michuano ya kimataifa nchini Tanzania.
Awali kipa huyo alikua anatakiwa na klabu ya Simba sc kuja kuchukua nafasi ya Moussa Camara lakini baada ya kipa huyo kuamua kusalia klabuni hapo kutokana na kocha Fadlu Davis kuamua kumtaka asalie kikosini humo amalizie kipengele cha kuongeza mwaka mmoja katika mkataba wake.
Fofana mwenye miaka 21 ni raia wa nchi ya Ivory Coast akiwa hana historia ya kuhamahama klabu ambapo alijunga na Al Hilal Fc mwaka 2022 akitokea San Pedro Fc ya nchini kwao Ivory Coast.
Kipa huyo ameenda Azam Fc kuchukua nafasi ya Mohamed Mustafa ambaye ametemwa klabuni hapo kutokana na kuandamwa na majeraha ya mara kwa mara ambapo sasa klabu hiyo itakua na makipa watatu akiwemo Fofana,Aishi Manula na Zubeiry Foba ambao watapambana kumshawishi kocha Frolent Ibenge kikosini humo nani awe chaguo la kwanza.
Ibenge anasuka kikosi muhimu kwa ajili ya msimu ujao akilenga kufanya vizuri kimataifa na ligi ya ndani msimu huu ambapo sasa ameshusha mastaa wa kutosha wa ndani na nje ya nchi kwa ajili ya kurejesha utawala wa Azam Fc ambao kwa sasa wana miaka zaidi ya kumi hawajachukua ubingwa wowote wa ndani wa ligi kuu wala michuano ya kimataifa.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Ibenge pia amefanya usajili wa mastaa wa kutosha kikosini humo ambapo amewasajili wachezaji wazoefu kama Himid Mao Mkami,Edward Charles Manyama,Jephte Kitambala,Pape Doudou Diallo,Aishi Manula na beki Lameck Lawi ambao moja kwa moja wataongeza uzoefu kikosini humo.
Moja ya kazi kubwa ya kwanza ya Ibenge ni kuhakikisha kuwa klabu hiyo inafanya vizuri katika ligi kuu ya ndani na nje ya nchi hasa katika michuano ya kimataifa ambapo haijawahi kuvuka hatua ya makundi hata mara moja katika historia ya klabu hiyo.
Katika michuano ya kimataifa msimu huu Azam Fc itaanzia hatua ya awali ya kombe la shirikisho ambapo itavaana na Al Merrekh ya Sudan mwezi septemba mwaka huu.