Kiungo mkabaji wa Simba Sc, Gerson Fraga atakuwa nje kwa wiki tatu hadi nne baada ya kupata majeraha ya goti siku ya Jumapili ilipocheza na Biashara United.
Taarifa hiyo imethibitishwa na mkuu wa idara ya mawasiliano wa Simba Sc,Haji Manara alipotembelea kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL) leo.
Manara amesema kuwa Fraga hatafanyiwa upasuaji bali atatibiwa kawaida na baada ya mwezi anatarajiwa kurudi uwanjani hivyo ataikosa pia mechi ya watani wa jadi itakayochezwa Oktoba 18,uwanja wa Benjamini Mkapa,Dar-es-salaam.