Site icon Sports Leo

Gamondi Anukia Apr Rwanda

Kocha wa zamani wa klabu ya Yanga sc raia wa Argentina mwenye umri wa miaka 58 Miguel Ángel Gamondi ameripotiwa kufanya mazungumzo na APR FC ya nchini Rwanda kwa ajili ya kuinoa klabu hiyo msimu ujao.

Ripoti kutoka nchini humo zinasema kuwa tayari makocha 38 wametuma maombi ya kazi katika klabu hiyo baada ya mchakato wa kutafuta kocha mpya kuanza.

Gamondi aliondoka nchini mwishoni mwa mwaka jana baada ya kushindwana na mabosi wa Yanga sc kufuatia mfululizo wa matokeo yasiyoridhisha ambapo hivi karibuni aliifundisha  katika timu ya Al Nasr nchini Libya.

Sasa mabosi wa Apr wana kazi kubwa ya kufanya mchujo ili kuamua nani atachukua kijiti cha kocha Darko Novic aliyeachana na klabu hiyo aliyodumu nayo takribani miezi 11.

Hata hivyo Gamondi pamoja na kupigiwa upatu kuchukua nafasi hiyo lazima ajipange kutokana na ukweli kwamba endapo atapata nafasi hiyo ajue timu za nchi huyo ni tofauti na za Tanzania ambazo zina bajeti kubwa ya usajili.

Exit mobile version