Mshambuliaji wa klabu ya Singida Black Stars Joseph Guede anatarajiwa kuukosa mchezo wa ligi kuu ya Nbc baina ya timu hiyo na Kmc utakaofanyika Septemba 12 katika uwanja wa Ccm Liti mjini Singida.
Guede ataungana na mastaa kama Jimson Mwinuke ambaye naye ana majeraha huku mastaa wengine kama Mohammed Camara na Maurouf Tchakei nao wataikosa mechi hiyo kutokana na kuchelewa kuripoti kutoka timu zao za Taifa.
Guede mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Yanga sc amejiunga na timu hiyo yenye makao yake makuu mkoani Singida baada ya kumaliza mkataba wake wa miezi sita Jangwani.
Singida Black Stars na Kmc zinatarajiwa kuwa na mchezo wenye upinzani mkali kutokana na vikosi hivyo kuwa na wachezaji mahiri sambamba na uchumi ulioimara tofauti na vilabu vingine ukiwatoa Simba sc,Azam Fc na Yanga sc.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Kocha Patrick Aussems na msaidizi wake Dennis Kitambi wana kazi kubwa ya kuhakikisha ushindi unapatikana kwa timu hiyo yenye alama sita ikicheza michezo miwili ya ligi kuu ya Nbc nchini.