Bodi ya ligi kuu ya Tanzania imetangaza kuwa vilabu vyote vinavyoshiriki ligi hiyo vimekubaliana kwa pamoja kuwa hakutakuwa na mechi itakayokuwa inachezwa pindi wawakilishi wa nchi katika mashindano mbalimbali ya kimataifa watakapokuwa wanacheza,hivyo ligi itakuwa inasimama kila kipindi hicho kikifika.
Hatua imekuja kuondoa tatizo la wingi wa mechi za viporo pindi timu za ndani zinapokuwa zinashiriki michuano mbalimbali ya CAF.
Mtendaji mkuu wa bodi ya ligi amesema kuwa wamefanya hivyo ili kumaliza changamoto ya mechi za viporo,hivyo hatua hiyo itaondoa kabisa na hakutakuwa tena viporo kwenye ligi hiyo.