Home Makala Halaand Kiboko

Halaand Kiboko

by Sports Leo
0 comments

Uongozi wa klabu ya Manchester City upo kwenye mazungumzo na mshambuliaji wao Erling Haaland juu ya kubadilisha vipingele vya mkataba wake hasa juu ya gharama ya kuvunja mkataba wa Erling Haaland inakadiriwa kufikia mpaka Paundi Milioni 174 ambazo ni sawa na Bilioni 461 za Kitanzania.

Sababu ya Maongezi hayo na mchezaji huyo ni kuhusishwa kwa baadhi ya viongizi wa Real Madrid kuanza mazungumzo ya chini na wakala wa mchezaji huyo hivyo kutokana na dau hilo inawezekana kabisa timu hiyo ikaweza kulipa kiasi hicho ili kumnasa staa huyo tishio kwa sasa.

Taarifa hizo zinakuja ikiwa ni wiki moja tangu Halaand aifunge Hattrick klabu ya Manchester United katika mchezo wa ligi kuu ambao United ilikubali kichapo cha jumla ya mabao 6-3 na staa huyo kuzua gumzo kutokana na kiwango hicho maridhawa.

banner

Halaand alijiunga na Manchester City akitokea Borrusia Dortmund kwa dau la paundi milioni 51 huku jumla usajili wake wote gharama zilifikia kiasi cha paundi milioni 85 na katika mkataba huo City iliweka kipengele cha kumuuza kwa dau la paundi milioni 171 ambacho kwa sasa kutokana na kiwango cha staa huyo pesa hiyo inaonekana ni kidogo na baadhi ya klabu kubwa kama Real Madrid na Manchester United zinaweza kulipa.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited