Hatimaye mshambuliaji Harry Kane ametwaa kombe lake la kwanza kwenye maisha yake ya soka baada ya Bayern Munich kutwaa ubingwa wa Bundesliga baada ya Bayer Leverkusen kulazimishwa sare ya 2-2 dhidi ya Freiburg zikiwa zimesalia mechi mbili pazia la ligi kuu ya Bundesliga kufungwa.
Bayern Munich ni Mabingwa wapya wa Bundesliga kwa kuwa pointi 76 walizonazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote ambapo hata kama Leverkusen watashinda mechi zao mbili zilizosalia hawawezi kuzifikia pointi za Bayern.
Ikimbukwe kuwa mshambuliaji huyo kiongozi wa timu ya Taifa ya Uingereza hajawahi kutwaa kombe lolote katika ngazi ya klabu tangu awe mchezaji rasmi wa kulipwa.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Kane kabla ya kujiunga na Bayern Munich ameichezea klabu ya Tottenham Fc kwa takribani miaka 11 ambapo hakutwaa taji lolote mpaka anajiunga na Bayern ambapo sasa ametwaa taji kwa mara ya kwanza.