Kiungo mshambuliaji wa Yanga,Bernard Morrison amerejesha leo mkataba wake kwa mabosi wake ambao ni kampuni ya GSM kupitia kwa Mkurugenzi wa uwekezaji Hersi Said baada ya kumalizana nao muda mrefu alipotua ndani ya Yanga.
Morrison alisaini mkataba huo wa miaka miwili mwezi Februari kabla ya mechi ya Machi 8 dhidi ya Simba ambapo alifunga bao pekee la ushindi dakika ya 44 lililoipa pointi tatu Yanga, Uwanja wa Taifa.
Morrison hakurudisha mkataba wake kwa mabosi wake ila leo ameamua kuuwasilisha baada ya tetesi kuwa ameingia kwenye anga za Simba ambao walikuwa wanaiwinda saini yake.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.