Home Makala “He is Back”

“He is Back”

by Sports Leo
0 comments

Staa wa Argentina Lionel Messi hatimaye atapata wasaa wa kuitumikia tena timu hiyo tangu alipofungiwa miezi mitatu na baraza la mpira wa miguu Amerika ya kusini(CoMEBALL) kufuatia kauli yake kuhusu kulishutumu baraza hilo kuhusu ufisadi.

Messi ataungana na Marcos Rojo na Sergio Aguero ambao nao wameitwa katika kikosi hichi kuelekea michezo ya kirafiki dhidi ya Brazil novemba 15 na novemba 18 atakutana na Uruguay nchini Israel huku marufuku yake ikifikia tamati novemba 3 hivyo kuwa na wasaa wa kushiriki michuano hiyo kwa mujibu wa mtandao wa twiter wa shirikisho la soka nchini Argentina.

Messi alikosa michezo minne ya timu ya taifa hilo wakati akitumikia adhabu ambapo timu hiyo ilishinda michezo miwili na kutoa sare miwili.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited