Klabu ya soka ya Azam Fc imekamilisha usajili wa kiungo wake mkabaji wa zamani Himid Mao Mkami (32) kutoka Klabu ya Ghazl El Mahalla ya Misri ambayo amemaliza nayo mkataba na kuwa huru.
Himid amemaliza mkataba wake na sasa nyota huyo anarejea tena nyumbani kwenye klabu yake ya zamani iliyomlea ya Azam FC kwa mkataba wa mwaka mmoja.
Kiungo licha ya kuwa alikuwa kwenye mazungumzo na Klabu ya Orlando Pirates ya Afrika kusini lakini Azam FC iliongeza ushawishi kwa kumpa ofa bora na kubwa kuliko wababe hao wa kwa madiba.
Himid aliondoka Azam FC mwaka 2018 na kujiunga na Klabu ya Project SC ya Misri Kisha ENPPI SC zote za Misri kabla ya kujiunga na Ghazl El Mahalla na sasa Amerejea tena Azam Fc kusaidia kurejesha ubabe wa vijana hao wa Chamazi ambao wamekua na wakati mgumu mbele ya Yanga sc na Simba sc kwa miaka tisa sasa wakiwa hawajachukua kombe lolote la ligi kuu.