Kocha Florent Ibenge ameachana na klabu ya As Vita ya nchini Congo baada ya kudumu kwa miaka tisa kama kocha mkuu klabuni hapo baada ya kuwa na msimu mibovu hivi karibuni,
Taarifa iliyotolewa na klabu hiyo na kuthibitishwa na Rais Bestine Kazadi imesomeka kama ifuatavyo “ ndugu mashabiki, ninatangaza kuondoka kwa kocha wetu Jean-Florent. Kwa niaba ya klabu ya AS Vita, tunamshukuru kwa utumishi wake na tunamtakia kila la kheri.”