Klabu ya Azam Fc imemtambulisha rasmi kocha Frolent Ibenge kama kocha mkuu mpya wa klabu hiyo akichukua nafasi ya kocha Rachid Taoussi ambaye mkataba wake umemalizika klabuni hapo msimu huu.
Ibenge amejiunga na Azam Fc baada ya kumaliza mkataba wake katika klabu ya Al Hilal Fc na moja kwa moja anakuja katika klabu hiyo kwa ajili ya kusuka upya kikosi kwa ajili ya msimu ujao.
Kocha huyo amesaini mkataba wa miaka miwili mbele ya mjumbe wa bodi ya klabu hiyo Abdulkareem Shermohamed ambapo sasa anaanza moja kwa moja kazi ya kusuka kikosi kwa kufanya usajili mkubwa.
Ibenge anakua mmoja ya makocha wanaolipwa vizuri zaidi nchini pengine mshahara wake haujawahi kulipwa na klabu yeyote nchini jambo ambalo kwa miaka kadhaa imewawia vigumu mabosi wa klabu ya Yanga sc na Simba sc kumchukua kocha huyo licha ya kumhitaji kwa nyakati tofauti tofauti.