Klabu ya Yanga sc siku chache baada ya kukamilisha usajili wa kiungo mshambuliaji raia wa Congo Dr Jonathan Ikangalombo kwa mkataba wa miaka miwili tayari imefanikiwa kumsajili staa huyo kwenye mfumo wa usajili wa klabu hiyo kwa ajili ya kutumika katika michezo mbalimbali.
Usajili wa Ikangalombo ulikua ukitarajiwa kukamilika muda wowote hasa baada ya staa huyo kuonekana uwanjani wakati Yanga sc ilipovaana na Tp Mazembe katika michuano ya klabu bingwa barani Afrika katika uwanja wa Benjamin Mkapa ambapo Yanga sc ilipata ushindi wa mabao 3-1.
Mbali na Ikangalombo pia klabu hiyo imefanikiwa kumuingiza kwenye mfumo beki Israel Mwenda baada ya kukamilisha usajili wake wiki chache zilizopita lakini klabu hiyo ilishindwa kuanza kumtumia baada ya kuwa kifungoni kutokana na adhabu ya Shirikisho la soka duniani (Fifa).
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Yanga sc ilifungiwa kufanya usajili kutokana na kushindwa kesi ya malipo ya mchezaji Augustine Okrah wa ghana baada ya kuachana nae bila kukamilisha taratibu za kimkataba.
Ikangalombo anatajwa kama winga mwenye kasi na anakuja kuongeza nguvu kwa Yanga sc hasa upande wa kulia ama kushoto ambapo tangu aondoke Jesus Moloko timu hiyo haijapata winga mwenye kasi.