Mshambuliaji nyota wa klabu ya Liverpool ya nchini Uingereza, Diogo Jota amelezwa kufariki dunia leo baada kupata ajali ya gari nchini Hispania mapema hii leo kulingana na ripoti za vyombo vya habari vya nchini humo.
Jota, mwenye umri wa miaka 28, alikuwa akitumia likizo yake katika nchi yake ya asili, Portugal kisha alielekea nchini humo kabla ya ajali hiyo kutokea katika mji wa Albacete ambapi alikua yeye pamoja na mdogo wake mwenye miaka 26 ambaye naye ni mchezaji wa timu ya Panafiel ya ligi ya madaraja ya chini nchini Ureno.
Klabu ya Liverpool bado haijatoa tamko lolote kuhusu tukio hilo, lakini vyombo vya habari vya Hispania, ikiwa ni pamoja na AS na Marca, vimeripoti kuwa gari lililokuwa likimchukua Jota lilipata ajali ya kutisha na kuua mchezaji huyo na dereva wake.
Jota alijiunga na Liverpool mwaka 2020 kutoka Wolverhampton Wanderers na alikuwa mchezaji muhimu katika kikosi cha Jurgen Klopp akisaidia timu hiyo kushinda kombe la FA na Carabao Cup.
Mashabiki wengi wa soka duniani wamekuwa wakituma ujumbe wa rambirambi kwa familia yake na kwa klabu ya Liverpool kufuatia kifo cha staa huyo aliyefunga ndoa siku tano zilizopita na kuacha mke na watoto watatu.